Wednesday, April 10, 2024
Basi moja lijulikano kwa jina la LUJIGA limepata ajali eneo la Malendi mpakani mwa mkoa wa Singida na mkoa wa Tabora, Basi hilo lifanyalo safari za Mwanza kwenda Dar es salaam lilipata ajali hiyo leo 10 April2024 katika eneo hilo majira ya saa 3 asubuhi likitokea Dar es salaam kwenda Mwanza baada ya kuligonga lori kwa nyuma kama linavyoonekana katika picha hapo juu. Hijafahamika mara moja idadi ya vifo wala majeruhi kutokana na ajali hilo mpaka hapo mamlaka husika zitakapotoa taarifa kamili. Lakini kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema idadi ya vifo ni kubwa na madhara ni makubwa katika ajali hiyo. Kadiri tutakavyoendelea kupata taarifa ndivyo tutakavyowaletea taarifa zaidi.
Tuesday, April 2, 2024
Mwalimu wa Shule ya Msingi Mbugani Kata ya Kiwanja, Herieth Lupembe na binti aliyekuwa akiishi naye ambaye ni mwananfunzi wa Kidato cha kwanza, Tatizo Haonga (16) wamekutwa wameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mwilini.
Mauaji hayo yamefanyika ndani ya nyumba aliyokuwa wakiishi pamoja na mtoto wa mwalimu huyo mwenye umri wa miaka mitano.
Mwanafunzi aliyeuawa pamoja na mwalimu huyo alikuwa anasoma katika Shule ya Sekondari Isenyela wilayani Chunya.
Katika tukio hilo, Haris Daud (5) anayesoma darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kengold amejeruhiwa na sasa anapatiwa matibabu katika Hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.
Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea jana Jumapili Machi 31, 2024 na majirani ndiyo waliobaini baada ya kutomuona mwalimu huyo akienda kanisani huku duka lake likiwa limefungwa, jambo ambalo si la kawaida.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Aprili mosi, 2024 jirani wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Merry Joel amesema walipoona duka limefungwa, waliamua kupiga simu ya mwalimu huyo ikawa inaita bila majibu.
Soma zaidi www.mwananchi.co.tz
Basi moja lijulikano kwa jina la LUJIGA limepata ajali eneo la Malendi mpakani mwa mkoa wa Singida na mkoa wa Tabora, Basi hilo lifanyalo...
-
Kuelekea mpambano wa ligi kuu soka Tanzania kati ya mnyama mkali simba sc na wana tamu tamu Mtibwa suger kesho 14/10/2017 ifuatayo ni histor...
-
Mvutano huu umeendelea kuwa mkubwa zaidi pale rais wa Marekani bwana Donald Trump alipoamua kumtolea lugha chafu mwenzake wa N.Korea bwana ...
-
Kuelekea mechi ya Mbao FC dhidi ya mnyama mkali Simba SC historia ya timu hizi ni kama ifuatavyo Timu hizi ktk historia zao zimekutana mara...