Monday, September 24, 2018

DERBY YA KARIAKOO, MPAMBANO MKALI KABISA WA WATANI WA JADI SIMBA Vs YANGA 30/09/2018


Kuelekea mpambano huu mkubwa barani Afrika Je wayajua mambo haya muhimu?       
 Huu ni mpambano wa kukata na shoka, ni miongoni mwa mipambano mikali zaidi barani Afrika ya watani wa jadi derby ukiacha mipambano kati ya Al ahly na Zamaleck za misri na ule wa Kaizer Chiefs na Orlando Pirates za Afrika kusini. Huu ni mpambano wa tatu kwa ukubwa barani Afrika. Ikumbukwe kuwa huu utakuwa ni mchezo wa 124 kama huna rekodi hiyo
    Katika michezo yote 123 iliyopita tangu mwaka 1965 rekodi zinaonyesha Simba imeitandika Yanga mara 44 na Yanga pia imeitandika simba mara 44 na wakenda sare mara 35 katika michezo yote zilivyokutana uso kwa uso. Pia ikumbukwe kuwa michezo hii yote 123 waliyowahi kukutana ni katika mashindano mbalimbali, ligi kuu Tanzania bara, ligi ya muungano wakati huo, kombe la FAT, Nyerere cup, Tusker cup, Hedex cup, klabu bingwa Afrika mashariki na kati kwa sasa Kagame cup, mtani jembe, mechi za kirafiki n.k.
    Katika mechi za ligi ligi kuu Tanzania bara peke yake utakuwa ni mchezo wa 101 ambapo katika michezo 100 iliyopita Yanga imeibuka wababe kwa simba kwa kuicharaza mara 35 huku simba ikiitandika Yanga mara 30 ilihali wakitoka sare mara 35. Kwa mantiki hiyo mechi hii huwa ni ya kusaka zaidi rekodi na kuweka heshima zaidi kuliko swala la pointi.
  Vile vile klabu hizi zote kila moja anatambia rekodi yake kwa mwenzake ambapo wengine wanasema tumebeba ubingwa mara nyingi zaidi na wenzao wanasema tunarekodi ya kushinda mabao mengi zaidi ktk mechi moja, lakini yote kwa yote tusubiri kuona nani ataibuka mbabe wa mwenzake. Kwetu sisi tuwaombee kila la kheri wote wacheze mchezo mzuri wa kiungwana bila kuwasahau waamuzi wazingatie vyema sheria za mchezo mwisho wa saa tupate mshindi aliyeshinda bila hila.

Friday, August 10, 2018

Ligi kuu ya Uingereza maarufu kama EPL kuanza leo rasmi

Ligi kuu ya uingereza EPL inatarajiwa kuanza leo rasmi kwa mchezo mmoja kati ya Manchester utd na Leicester city mchezo utakaochezwa majira ya saa 4.00 usiku kwa saa za Afrika mashariki. Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo kazaa ambapo mechi kubwa inayosubiriwa kwa hamu ni ya jumapili kati ya mabingwa watetezi Manchester city na Arsenal mechi ya kisasi. Mashabiki wanasubiri kuona Arsenal italipa kisasi cha kuchapwa mechi 3 msimu uliopita au itaendelea kuwa mteja wa sky blue the City.

Wednesday, May 9, 2018

Uharibifu mkubwa ulosababishwa na Volcano jimboni Hawii Marekani

Huu ni uharibifu mkubwa sana ulioletwa na volcano katika jimbo la Hawii, volcano hiyo iliyolipuka juzi imeleta uharibifu mkubwa sana ukiwa haujapoteza maisha ya watu wala kujeruhi, lakini umeleta uharibifu wa makazi pamoja na mali zingine nyingi kiasi cha kushangaza wakazi hao wa Hawaii. Ni miongoni mwa milipuko mibaya kabisa ya volcano kuwa kuikumba Marekani. Picha kwa hisani ya BBC

Sunday, May 6, 2018

Tarehe kama ya leo katika historia (May 06)

           Tarehe kama ya leo mwaka 2012 ilipigwa mechi kubwa ya watani wa jadi simba ikimkaribisha Yanga katika uwanja wa taifa Dar es salaam. Hii ilikuwa ni miongoni mwa mechi ya watani iliyokuwa na mabao mengi kabisa ukiacha ile ya 01/06/1968 na ile ya 19/07/1977 ambayo rekodi yake haijavunjwa hadi leo
         
          Mechi hii ya May 06,2012 simba iliikung'uta Yanga bao 5-0.
Bao la kwanza likiwekwa wavuni na Emmanuel Okwi dakika ya 2 tu ya mchezo huku Felix Sunzu Mzambia huyu akiweka kambani bao la pili kwa njia ya penalti dakika ya 56 ya mchezo.Dakika ya 62 ya mchezo Emmenuel Okwi tena akarudi kambani kwa mara ingine kuweka bao la tatu kufuatia uzembe wa mabeki wa yanga, huku Juma Kaseja akipachika bao la nne kwa njia ya penalti dakika ya 67 ya mchezo. Patrick Mutesa Mafisango akamalizia karamu ya magoli baada ya kuzifumania nyavu za Yanga katika dakika ya 72 ya mchezo na kuufanya mchezo uishie kwa 5-0 na kuifanya simba kubeba ubingwa msimu huo.

Friday, May 4, 2018

Ugeni uliotembelea Stendi kuu ya mabasi Singida (Misuna Terminal) toka Jumatano na Ijumaa East Africa Radio/EATV (channel5)


      Ugeni huu wa East Africa radio na EATV ulitembelea kufanya mahojiano maalumu na uongozi wa stand kuu ya Misuna Terminal pamoja na wadau wa michezo wa misuna Terminal kutokana na kuvutiwa kwao na mambo mkubwa mawili
       1. Kutokana na mpangilio,utaratibu na nidhamu ya hali ya juu ndani ya stand hii,                walilazimika kuutafuta uongozi wa umoja wa mawakala angalau kupata darasa ni mbinu zipi au ni mambo gani yalifanyika kudhibiti mpangilio huu, utaratibu huu na nidhamu hii ya hali ya juu ambayo kwa mujibu wa maelezo ya wageni hawa hawajawahi kukutana na jambo kama hili stendi zote Tanzania. Ni jambo lisilopinginga kuwa ni kweli stendi nyingi Tanzania kama si zote hazina utaratibu mzuri wa kuhudumia jamii na kusababisha kero kubwa kwa wasafiri na watumiaji mbali mbali wa stendi hizo kiasi cha kusababisha kuitwa waizi, wahuni na walevi. Lakini kwa upande wa Stendi ya Singida Misuna Terminal, hili ni tofauti kabisa kiasi kwamba wageni hawa kuusifia sana kwa uongozi wa umoja wa mawakala kusimamia vyema utaratibu huu na nidhamu kwa wahudumu. Hivyo shukurani nyingi kwa wageni hawa East Africa Radio na EATV kwa kuliona hili na kuthamini jambo hili jema waliloliona na kuwajulisha umma wa Africa mashariki. Linaweza kuwa ni jambo la kuigwa na wengine kuondoa dhana mbaya kwa sekta hiyo ya huduma ya usafirishaji
       2. Kutokana na kuvutiwa na idadi kubwa ya wadau wa michezo na washabiki wengi wa michezo na pia kujua maendeleo ya klabu ya Misuna Stand Football Club ambayo inamilikiwa na umoja wa mawakala,East Africa Radio/EATV walifanya mahojiano mbali mbali na viongizi wa chama cha soka cha wilaya, viongozi wa Misuna stand FC pamoja na wadau mbali mbali wa michezo waliokuwepo.Hata hivyo wadau wa michezo walifurahia ugeni huu kupitia kipindi chao cha KIPENGA EXTRA na kuomba watembelee mara kwa mara kwa maendeleo ya michezo nchini. Mapokezi ya wageni hawa yalienda vizuri na wadau wa michezo washukuru sana ujio huu wa ugeni kutoka East Africa Radio kwa kuwatembelea na kufanya ziara hizi mikoani kwa malengo ya kuibua changamoto mbali mbali na kuibua vipaji mbali mbali kama vipo.

Sunday, April 29, 2018

SIMBA YAIPA KIPIGO YANGA KATIKA MECHI YA 100 YA LIGI KUU TOKA 1965 IKIZIKUTANISHA TIMU HIZI.

Ilikuwa ni dakika ya 37 Erasto Edward Nyoni alipoipatia Simba bao pekee lililotosha kuwaadhibu watani wao wa jadi kufuatia uzembe wa mabeki wa Yanga walioshindwa kuundoa mpira wa mkwaju wa adhabu ndogo uliopigwa na Shiza Kichuya nje kidogo ya goal la yanga pale ulipoparazwa kichwa na walinzi wa Yanga na kumkuta Erasto Nyoni na kuukwamisha wavuni kwa kichwa. Simba waliuanza mchezo huo kwa kasi na umakini mkubwa na tahadhari kwakuwahofia wapinzani wao pia.
     Iliwachukua dakika 37 Simba kupachika bao hilo moja kutokana faulo aliyochezewa kapombe. Hata hivyoYanga walicheza mchezo mzuri na wa kuvutia pamoja na kupungua kwa Hassan Kessy aliyelimwa kadi ya pili ya njano dakika ya pili tu ya kipindi cha pili. Mpaka mwisho simba ikamaliza kwa ushindi wa bao hilo moja na kufikisha point 62 pointi 14 juu ya Yanga na kupata nafasi nzuri zaidi ya kuusogelea ubingwa ikihitaji pointi 5 tu ktk mechi zake 4 ilizobakiza ili kutawazwa kuwa mabingwa wa Tanzania bara
     Huu ni mchezo wa 100 wa ligi kuu toka zimeanza kukutana timu hizi kuanzia mwaka 1965 ukiacha mechi za kirafiki na mashindano mengine. Ktik mechi zote hizi 100 za lihi kuu yanga ndio kinara wa kuifunga simba pale ilipofanikiwa kuifunga mara 35 na simba imeshinda mara 30 na zinazosalia ni sare.

Wednesday, April 25, 2018

KUELEKEA MPAMBANO WA WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA 29/04/2018 MCHEZO WA 123 BAINA YAO


Hii ni mechi kubwa sana katika ukanda wa afrika mashariki ni derby ya tatu kwa ukubwa Afrika baada ya ile ya Al ahly na Zamaleck huko Misri na ile ya Kaizer chiefs vs Orlando pirates. Ikumbukwe kuwa timu hizi toka zimeanza kukutana uso kwa mara 122 toka mwaka 1965 mpaka hii leo katika mechi mbali mbali zikiwemo za kirafiki, ligi na mashindano mengine mbali mbali.
    Katika michezo yote 122 waliyocheza Yanga imefanikiwa kuitandika simba mara 44 wakati Simba ikiichapa Yanga mara 43 ilihali wakienda sare mara 35. Chakusubiri ni kuona nani ataibuka na ushindi katika mpambano huo wa 123 wa kukata na shoka. Timu zote tuzitakie kila la kheri katika mpambano huo

Monday, January 29, 2018

HAWA NDIO WABABE WA SOKA LA BONGO NA REKODI ZAO LUKUKI. JE KUNA DALILI ZOZOTE ZA KUFANYA MAPINDUZI YA SOKA TANZANIA ILI NA VILABU VINGINE VITAWALE SOKA LA TANZANIA?


Hawa ndio wababe wa soka la bongo wenye historia kubwa kabisa ya soka letu la bongo,bado hatujaona dalili zozote za kufanyika mapinduzi ya soka Tanzania kuondoa ama kupunguza utawala wa wababe hawa wa soka la bongo Simba na Yanga japo tunatamani sana kuona mapinduzi hayo ya soka kama ilivyotokea huko kenya na Uganda ambapo utawala wa vilabu kama Kenya breweries,AFC Leopards,Gormahia na zikatokea timu kama Tusker, sofapaka na zingine zinazotishia kuondoa kabisa utawala wa vilabu vikongwe. Uganda pia kulikuwa na Sports club villa, The Express na sasa utawala wao tayari umeshaporwa na vilabu kama URA,KCC na zingine. Lakini kwa Tanzania bado hali hii ya mapinduzi ya soka haijajitokeza sana japo kuna vilabu kama Azam na singida united,Mtibwa n.k. lakini bado havitishii utawala wa soka wa wababe hawa Simba na Yanga
         Wababe hawa wa soka la bongo wenyewe kwa wenyewe wameshakutana uso kwa uso mara 122 katika mashindano mbali mbali ya kitaifa kimataifa na mechi za kirafiki toka mwaka 1965. Katika mapambano yote hayo Yanga wamefanikiwa kuibamiza simba mara 44 wakati simba nao wakichapa yanga mara 43 na wakaenda sare mara 35 mpaka mchezo wa mwisho wa ligi kuu uliochezwa October 28 ulioishia kwa sare ya 1-1.
        Mashindano walioshiriki wababe hawa na kuchukua kombe ni kama ifuatavyo
1.Klabu bingwa afrika mashariki na kati/ kagame cup
      Simba 6
      Yanga 5
2.Ligi kuu
     Simba 18
     Yanga 27
3.Muungano cup
      Simba 5
      Yanga 6
4. FAT cup
      Simba 1
      Yanga 4
5.Tusker cup
    Simba 5
    Yanga 2
6.Mapinduzi cup
   Simba 3
  Yanga 1
7.Ngao ya jamii
    Simba 3
    Yanga 4
8.Mtani jembe
     Simba 2
     Yanga 0

Tuesday, January 23, 2018

KUELEKEA MPAMBANO WA AZAM V YOUNG AFRICANS JE WAJUA HAYA?

Kuelekea dabi hii ndogo ya Dar es salaam hizi ni takwimu chache tu kuhusu historia za kukutana kwao hizi timu. Azam wameingia VPL msimu wa 2008/2009 wakati yanga ipo ligi kuu tangu mwaka 1965. Timu hizi zimekutana mara 28 ktk michezo tofauti tofauti ikiwemo ligi kuu, FA, mapinduzi cup, na hata Kagame cup. Tangu zimeanza kukutana Dar Young Africans wametandika Azam Fc mara 10 huku Azam pia ikiichapa yanga mara 10 pia na michezo 8 iliyobaki walikwenda sare. Kwavile takwimu zao zinafanana tunachosubiri sisi ni kuona nani ataibuka kidedea katika mchezo wao wikiendi hii.

Sunday, January 21, 2018

KUELEKEA MPAMBANO WA KAGERA SUGAR VS SIMBA SC KAITABA LEO 22/01/2018

Timu hizi katika historia yao zimekutana uso kwa uso mara 17 na Simba sports club mnyama mkali kuibuka mbabe kwa kuibandua Kagera suger wakata miwa mara 9 ilihali wakata miwa hao wakiukata mkia wa mnyama 2 huku wakienda sare mara 6. Mpambano huu ni wa kukata na shoka ukizingatia mnyama mkali anataka kujidhatiti kileleni hadi ubingwa wakati huo kagera sugar ikikwepa mkasi wa kushuka daraja. Je nani anaibuka mbabe wa leo. Tusubiri dakika 90

Wednesday, January 10, 2018

KUELEKEA PAMBANO LA SIMBA SC V SINGIDA UNITED JE WAJUA?

Timu hizi zimekutana mara 3 mpaka sasa, Simba wamefanikiwa kuwafunga Singida united mara mbili katika moja ya mechi ya ligi kuu miaka ya 2000 huku ikiifunga ktk mechi ya FA msimu wa 2015/2016 . Singida united iliifunga simba ktk mechi ya marudiano ya ligi kuu Namfua bao 1-0 mwaka wa 2000 huku ikiichapa Yanga pia bao 1-0 na pia Prisons bao 1-0 msimu huo huo.
Tuwaachie wao watuamulie mechi hii inayofuata nani atakuwa mbabe.

  Basi moja lijulikano kwa jina la LUJIGA  limepata ajali eneo la Malendi mpakani mwa mkoa wa Singida na mkoa wa Tabora, Basi hilo lifanyalo...