Thursday, September 28, 2017

KUELEKEA MPAMBANO WA STAND UTD Vs SIMBA SC, ZIFUATAZO NI REKODI FUPI ZA HISTORIA YAO

Timu hizi hazina historia kubwa sana ya kukutana katika soka la Tanzania, Stand united maarufu kama chama la wana si timu mwenyeji sana ktk ligi kuu Vodacom ikiwa kama na misimu mitatu tu iliyopita.
          Toka Stand united kuingia ligi kuu vodacomTanzania timu hizi zimekutana mara 6 katika mechi za ligi kuu vodacom Tanzania, hawajawahi kukutana ktk mechi zingine tofauti ma ligi kuu bara
Simba sports club maarufu kama mnyama mkali imewaadhibu chama la wana Stand United mara 5 ilihali Chama la wana Stand united walifanikiwa kuicharaza simba mnyama mkali mara 1 katika mechi zote walizowahi kukutana.
       Hivyo basi tusubiri katika mchezo huu unaokuja, Je chama la wana watafuta uteja kwa mnyama mkali au Mnyama mkali ataendeleza ubabe wake kwa chama la wana?

Sunday, September 24, 2017

YAWEZA IKAWA NDIO MECHI YA KIBABE ZAIDI DUNIANI KAMA SI MIONGONI MWA MECHI ZA KIBABE SANA DUNIANI

Mechi hii ilichezwa jana tarehe 23/09/2017 kati ya FENERBAHCE Vs BESIKTAS katika ligi kuu ya UTURUKI. Mechi hii ambayo Fenerbahce ilishinda kwa mabo mawili kwa moja ilishuhudia ubabe wa hali ya juu kuliko uliowahi kutokea. Mechi ilishuhudia kadi 11 za njano huku mbili zikigeuka kuwa Kadi nyekundu na kufanya idadi ya kadi yekundu kuwa 4 katika mchezo mmoja. Mchezo ulichezwa wa kibabe sana.
V.Jassen wa Fenerbahce alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 23
O.Ozyakup wa Besiktas pia alikula njano dakika hiyo hiyo ya 23
M.Ekici wa Fenerbahce alikula njano dakika ya 30 huku
A.Hutchinson wa Besiktas naye akila njano dakika ya 36
    Dakika ya 41 Ricardo Quaresma wa Besiktas alikula njano yake naye huku dakika ya 43 huyo huyo Quaresma alikula njano ya pili nakuonyeshwa Red kadi ya kwanza.
Neto wa Fenerbahce alikula kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 45 na kufanya kadi nyekundu kuwa mbili ktk mchezo
Dakika ya 77 A. Potuk wa Fenerbahce naye alikula njano huku dakika moja tu baadaye yaani dakika ya 78 D.Tusic wa Besiktas akila na yeye njano yake
Katika dakika ya 80 I. Koybasi wa Fenerbahce alikula kadi nyekundu ya moja kwa moja na kufanya kadi nyekundu kuwa tatu katika mchezo ili hali dakika ya 85 A. Hutchinson wa Besiktas akipewa kadi ya njano ya pili na kuonyeshwa nyekundu kuufanya mchezo kuwa na kadi 4 nyekundu mbili kila upande
Dakika ya 93 R. Babel wa Besiktas alipewa naye kadi ya njano huku Alvaro Negredo wa Besiktas hiyo hiyo nayo akihitimisha mgao wa kadi dakika ya 95 naye kupewa njano yake
        Hivyo mchezo ulimalizika kwa idadi ya kadi 11 za njano mbili zikigeuka kadi nyekundu na kadi nyekundu mbili za moja kwa moja kufanya idadi ya kadi nyekundu 4. Jumla kadi 13 zilitoka katika mchezo mmoja.

MVUTANO MKUBWA KATI YA N.KOREA NA MAREKANI


Mvutano huu umeendelea kuwa mkubwa zaidi pale rais wa Marekani bwana Donald Trump alipoamua kumtolea lugha chafu mwenzake wa N.Korea bwana Kim Un kwa kumuita mwendawazimu(madman) na na ni mtu mwenye kutaka kujiua mwenyewe mtu wa mabomu, na amejitapa kuiangamiza kabisa N.Korea maneno yaliyowakasirisha sana watawala wote wa Pyongyang na kumfunya Rais Kim Un kuyajibu maneno hayo kwa kejeli kubwa sana kwa kumuita Trump kuwa ni kichaa na mbwa anayebweka tu. Kubweka kwa mbwa hakunizuii kuendelea kufanya majaribio yangu ya silaha. Rais kim Un ameahidi kutekeleza jaribio kubwa la bomu la hydrogen ambalo halijawahi kutokea ktk bahari ya pacific na amemwambia Trump kuwa matusi yake aliyomtukana atayalipia gharama kubwa sana. Hatuelewi wataalam wa mambo nyie mnatathimini vipi hili.

Sunday, September 17, 2017

KUELEKEA MECHI YA LIGI KUU JUMAMOSI KATI YA SMBA SC Vs MBAO FC HISTORIA YAO

Kuelekea mechi ya Mbao FC dhidi ya mnyama mkali Simba SC historia ya timu hizi ni kama ifuatavyo
Timu hizi ktk historia zao zimekutana mara 3 ktk mechi tofauti tofauti. Katika mechi hizo 3 zilizokutana simba sports club imeshinda zote ilihali mbao FC wamepoteza mechi zote tatu,
Mechi ya kwanza zilikutana ktk mchezo wa ligi kuu vodacom msimu wa 2016/17 katika uwanja wa taifa ambapo simba waliibuka na ushindi wa bao 1 bila bao lilofungwa dakika ya 86
Katika mechi ya pili timu hizi zilikutana ktk mchezo wa marudiani ligi kuu ndani ya uwanja wa CCM KIRUMBA simba ikitoka kuadhibiwa na Kagera sugar. Katika mchezo huu Simba waliibuka na ushindi wa bao 3 kwa 2 ikitoka nyuma ya mabao mawili. Mabao ya simba yalifungwa na Fredrick Blagnon dakika ya 81 na 89 wakati Mzamiru Yasin akimalizia la tatu katika dakika ya 92 kuhitimisha ushindi wa 3-2
Mechi ya tatu zilikutana May 27,2017 ktk mchezo wa fainali ya AZAM FEDERATION CUP ambapo simba iliibuka pia na ushindi wa bao 2 kwa 1 mabao yaliyofungwa na Fredrick Blagnon na la pili Shiza kichunya kwa njia ya penalti baada ya mlinzi mmoja wa mbao kuunawa mpira. Je mechi hii itaendelea kuwabeba simba au Mbao watavunja mwiko wa kufungwa? Tusubiri dakika 90 zitatuamulia.

KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA DHIDI YA MWADUI FC LEO 17/09/2017

1. Aish manula
2. Ally shomari
3. Zimbwe Jr
4. Salim mbonde
5. Juuko mursheed
6. James Kotei
7. Yahaya Ramadhani kichuya
8. Mzamiru Yasin
9. John Boko Adebayor
10. Niclaus Gyan
11. Emmanuel Okwi

Kwa kupata habari na matukio mbali mbali

Tunajaribu kuweka sawa blog hii ili iwaletee habari, taarifa mbali mbali na matukio ya kijamii

  Basi moja lijulikano kwa jina la LUJIGA  limepata ajali eneo la Malendi mpakani mwa mkoa wa Singida na mkoa wa Tabora, Basi hilo lifanyalo...