Wednesday, April 10, 2024


  Basi moja lijulikano kwa jina la LUJIGA  limepata ajali eneo la Malendi mpakani mwa mkoa wa Singida na mkoa wa Tabora, Basi hilo lifanyalo safari za Mwanza kwenda Dar es salaam lilipata ajali hiyo leo 10 April2024 katika eneo hilo majira ya saa 3 asubuhi likitokea Dar es salaam kwenda Mwanza baada ya kuligonga lori kwa nyuma kama linavyoonekana katika picha hapo juu. Hijafahamika mara moja idadi ya vifo wala majeruhi kutokana na ajali hilo mpaka hapo mamlaka husika zitakapotoa taarifa kamili. Lakini kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema idadi ya vifo ni kubwa na madhara ni makubwa katika ajali hiyo. Kadiri tutakavyoendelea kupata taarifa ndivyo tutakavyowaletea taarifa zaidi.

Tuesday, April 2, 2024



Mwalimu wa Shule ya Msingi Mbugani Kata ya Kiwanja, Herieth Lupembe na binti aliyekuwa akiishi naye ambaye ni mwananfunzi wa Kidato cha kwanza, Tatizo Haonga (16) wamekutwa wameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mwilini.

Mauaji hayo yamefanyika ndani ya nyumba aliyokuwa wakiishi pamoja na mtoto wa mwalimu huyo mwenye umri wa miaka mitano.

Mwanafunzi aliyeuawa pamoja na mwalimu huyo alikuwa anasoma katika Shule ya Sekondari Isenyela wilayani Chunya.

Katika tukio hilo, Haris Daud (5) anayesoma darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kengold amejeruhiwa na sasa anapatiwa matibabu katika Hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea jana Jumapili Machi 31, 2024 na majirani ndiyo waliobaini baada ya kutomuona mwalimu huyo akienda kanisani huku duka lake likiwa limefungwa, jambo ambalo si la kawaida.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Aprili mosi, 2024 jirani wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Merry Joel amesema walipoona duka limefungwa, waliamua kupiga simu ya mwalimu huyo ikawa inaita bila majibu.

Soma zaidi www.mwananchi.co.tz

Tuesday, February 21, 2023

 TAHADHARI YA KIMBUNGA

Mamlaka ya Madagascar ilisema siku ya Jumatatu kuwa takriban watu milioni mbili wataathirika mara tu Kimbunga Freddy kitakapotua katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Wataalamu kutoka Ofisi ya taifa ya Majanga wametabiri kuwa kimbunga hicho kitakumba mikoa tisa nchini huo.

Vikosi vya dharura vinajiandaa kukabiliana na mvua kubwa, mafuriko na hata maporomoko ya ardhi katika maeneo ambayo yataathiriwa.

Kimbunga hicho kimekuwa kikikumba bahari ya Hindi kwa wiki kadhaa na kwa mujibu wa wataalamu, athari zake zitaonekana kati ya wilaya za Vatomandry kusini-mashariki na Manakara ambayo iko pwani ya mashariki.

Wale wanaoishi katika maeneo hayo wameshauriwa kuimarisha milango na paa zao, kukata miti hatari na kubaki nyumbani wakati wa kimbunga hicho.

Taifa hilo la kisiwa ni miongoni mwa nchi 10 za juu zaidi barani Afrika zilizoathiriwa zaidi na vimbunga na hatari kwa majanga, kulingana na Mpango wa Chakula Duniani, Dhoruba la awali ya kitropiki iliyoikumba nchi ilikuwa Cheneso, iliyopiga Januari mwaka huu. Takriban watu 30 walikufa na zaidi ya 40,000 walikimbia makazi yao.



Sunday, February 19, 2023

MECHI ZA MAKUNDI ROUND YA PILI YA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRICA ZAMALIZKA

 Mechi za makundi za round ya pili ya kombe la shirikisho zimemalizaka muda mchache uliopita  ambapo matokeo ya mechi hizo ni kama yafuatayo

st Eloi Lupopo ya DRC imekubali kichapo cha bao 2-1 mbele ya Mrumo ya Africa kusini wakati waarabu wa El Akhdar ya Libya na USM Alger ya Algeria wametoka sare ya bao 1-1 jijini Tripoli Libya

Waarbu wa Misri pia Future FC na Pyramids wamekwenda sare ya bao 1-1 nyumbani kwa FutureFC

Real Bamako na Monistir ya Tunisia pia wametoka sare ya bao 1-1 jijini Bamako Mali ilihali Rvers UTD imeichapa Asec Memosas ya ya Ivory coast 3-0 jijini Lagos wakati Young Africans ya Tanzania ikiibugiza TP Mazembe ya DRC mabao 3-1 jijini Dar es salaam

mechi zingine zinazoendelea sasahivi ni FAR Rabat ya Moroco ikimenyana na Kara ya Togo  jijini Rabat huku FAR Rabat ikiibuka na ushindi wa bao 5-1 wakati DC.Motema pembe ya DRC ikienda sare ya bila kufungana na Diables ya Congo Brazavile jijini Lubumbashi,.

Sunday, January 9, 2022

KOMBE LA MAPINDUZI 2022

 Kombe la mapinduzi msimu wa 2022 linafikia hatua ya nusu fainali kesho kwa michezo miwili ya nusu fainali ambapo,

YANGA itakwaana na AZAM FC,wakati wekundu wa msimbazi mnyama SIMBA SC atakwaana na NAMUNGO FC

Monday, September 24, 2018

DERBY YA KARIAKOO, MPAMBANO MKALI KABISA WA WATANI WA JADI SIMBA Vs YANGA 30/09/2018


Kuelekea mpambano huu mkubwa barani Afrika Je wayajua mambo haya muhimu?       
 Huu ni mpambano wa kukata na shoka, ni miongoni mwa mipambano mikali zaidi barani Afrika ya watani wa jadi derby ukiacha mipambano kati ya Al ahly na Zamaleck za misri na ule wa Kaizer Chiefs na Orlando Pirates za Afrika kusini. Huu ni mpambano wa tatu kwa ukubwa barani Afrika. Ikumbukwe kuwa huu utakuwa ni mchezo wa 124 kama huna rekodi hiyo
    Katika michezo yote 123 iliyopita tangu mwaka 1965 rekodi zinaonyesha Simba imeitandika Yanga mara 44 na Yanga pia imeitandika simba mara 44 na wakenda sare mara 35 katika michezo yote zilivyokutana uso kwa uso. Pia ikumbukwe kuwa michezo hii yote 123 waliyowahi kukutana ni katika mashindano mbalimbali, ligi kuu Tanzania bara, ligi ya muungano wakati huo, kombe la FAT, Nyerere cup, Tusker cup, Hedex cup, klabu bingwa Afrika mashariki na kati kwa sasa Kagame cup, mtani jembe, mechi za kirafiki n.k.
    Katika mechi za ligi ligi kuu Tanzania bara peke yake utakuwa ni mchezo wa 101 ambapo katika michezo 100 iliyopita Yanga imeibuka wababe kwa simba kwa kuicharaza mara 35 huku simba ikiitandika Yanga mara 30 ilihali wakitoka sare mara 35. Kwa mantiki hiyo mechi hii huwa ni ya kusaka zaidi rekodi na kuweka heshima zaidi kuliko swala la pointi.
  Vile vile klabu hizi zote kila moja anatambia rekodi yake kwa mwenzake ambapo wengine wanasema tumebeba ubingwa mara nyingi zaidi na wenzao wanasema tunarekodi ya kushinda mabao mengi zaidi ktk mechi moja, lakini yote kwa yote tusubiri kuona nani ataibuka mbabe wa mwenzake. Kwetu sisi tuwaombee kila la kheri wote wacheze mchezo mzuri wa kiungwana bila kuwasahau waamuzi wazingatie vyema sheria za mchezo mwisho wa saa tupate mshindi aliyeshinda bila hila.

Friday, August 10, 2018

Ligi kuu ya Uingereza maarufu kama EPL kuanza leo rasmi

Ligi kuu ya uingereza EPL inatarajiwa kuanza leo rasmi kwa mchezo mmoja kati ya Manchester utd na Leicester city mchezo utakaochezwa majira ya saa 4.00 usiku kwa saa za Afrika mashariki. Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo kazaa ambapo mechi kubwa inayosubiriwa kwa hamu ni ya jumapili kati ya mabingwa watetezi Manchester city na Arsenal mechi ya kisasi. Mashabiki wanasubiri kuona Arsenal italipa kisasi cha kuchapwa mechi 3 msimu uliopita au itaendelea kuwa mteja wa sky blue the City.

  Basi moja lijulikano kwa jina la LUJIGA  limepata ajali eneo la Malendi mpakani mwa mkoa wa Singida na mkoa wa Tabora, Basi hilo lifanyalo...