Kuelekea mechi ya Mbao FC dhidi ya mnyama mkali Simba SC historia ya timu hizi ni kama ifuatavyo
Timu hizi ktk historia zao zimekutana mara 3 ktk mechi tofauti tofauti. Katika mechi hizo 3 zilizokutana simba sports club imeshinda zote ilihali mbao FC wamepoteza mechi zote tatu,
Mechi ya kwanza zilikutana ktk mchezo wa ligi kuu vodacom msimu wa 2016/17 katika uwanja wa taifa ambapo simba waliibuka na ushindi wa bao 1 bila bao lilofungwa dakika ya 86
Katika mechi ya pili timu hizi zilikutana ktk mchezo wa marudiani ligi kuu ndani ya uwanja wa CCM KIRUMBA simba ikitoka kuadhibiwa na Kagera sugar. Katika mchezo huu Simba waliibuka na ushindi wa bao 3 kwa 2 ikitoka nyuma ya mabao mawili. Mabao ya simba yalifungwa na Fredrick Blagnon dakika ya 81 na 89 wakati Mzamiru Yasin akimalizia la tatu katika dakika ya 92 kuhitimisha ushindi wa 3-2
Mechi ya tatu zilikutana May 27,2017 ktk mchezo wa fainali ya AZAM FEDERATION CUP ambapo simba iliibuka pia na ushindi wa bao 2 kwa 1 mabao yaliyofungwa na Fredrick Blagnon na la pili Shiza kichunya kwa njia ya penalti baada ya mlinzi mmoja wa mbao kuunawa mpira. Je mechi hii itaendelea kuwabeba simba au Mbao watavunja mwiko wa kufungwa? Tusubiri dakika 90 zitatuamulia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Basi moja lijulikano kwa jina la LUJIGA limepata ajali eneo la Malendi mpakani mwa mkoa wa Singida na mkoa wa Tabora, Basi hilo lifanyalo...
-
Kuelekea mpambano wa ligi kuu soka Tanzania kati ya mnyama mkali simba sc na wana tamu tamu Mtibwa suger kesho 14/10/2017 ifuatayo ni histor...
-
Mvutano huu umeendelea kuwa mkubwa zaidi pale rais wa Marekani bwana Donald Trump alipoamua kumtolea lugha chafu mwenzake wa N.Korea bwana ...
-
Kuelekea mechi ya Mbao FC dhidi ya mnyama mkali Simba SC historia ya timu hizi ni kama ifuatavyo Timu hizi ktk historia zao zimekutana mara...
No comments:
Post a Comment