Mechi hii ilichezwa jana tarehe 23/09/2017 kati ya FENERBAHCE Vs BESIKTAS katika ligi kuu ya UTURUKI. Mechi hii ambayo Fenerbahce ilishinda kwa mabo mawili kwa moja ilishuhudia ubabe wa hali ya juu kuliko uliowahi kutokea. Mechi ilishuhudia kadi 11 za njano huku mbili zikigeuka kuwa Kadi nyekundu na kufanya idadi ya kadi yekundu kuwa 4 katika mchezo mmoja. Mchezo ulichezwa wa kibabe sana.
V.Jassen wa Fenerbahce alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 23
O.Ozyakup wa Besiktas pia alikula njano dakika hiyo hiyo ya 23
M.Ekici wa Fenerbahce alikula njano dakika ya 30 huku
A.Hutchinson wa Besiktas naye akila njano dakika ya 36
Dakika ya 41 Ricardo Quaresma wa Besiktas alikula njano yake naye huku dakika ya 43 huyo huyo Quaresma alikula njano ya pili nakuonyeshwa Red kadi ya kwanza.
Neto wa Fenerbahce alikula kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 45 na kufanya kadi nyekundu kuwa mbili ktk mchezo
Dakika ya 77 A. Potuk wa Fenerbahce naye alikula njano huku dakika moja tu baadaye yaani dakika ya 78 D.Tusic wa Besiktas akila na yeye njano yake
Katika dakika ya 80 I. Koybasi wa Fenerbahce alikula kadi nyekundu ya moja kwa moja na kufanya kadi nyekundu kuwa tatu katika mchezo ili hali dakika ya 85 A. Hutchinson wa Besiktas akipewa kadi ya njano ya pili na kuonyeshwa nyekundu kuufanya mchezo kuwa na kadi 4 nyekundu mbili kila upande
Dakika ya 93 R. Babel wa Besiktas alipewa naye kadi ya njano huku Alvaro Negredo wa Besiktas hiyo hiyo nayo akihitimisha mgao wa kadi dakika ya 95 naye kupewa njano yake
Hivyo mchezo ulimalizika kwa idadi ya kadi 11 za njano mbili zikigeuka kadi nyekundu na kadi nyekundu mbili za moja kwa moja kufanya idadi ya kadi nyekundu 4. Jumla kadi 13 zilitoka katika mchezo mmoja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Basi moja lijulikano kwa jina la LUJIGA limepata ajali eneo la Malendi mpakani mwa mkoa wa Singida na mkoa wa Tabora, Basi hilo lifanyalo...
-
Kuelekea mpambano wa ligi kuu soka Tanzania kati ya mnyama mkali simba sc na wana tamu tamu Mtibwa suger kesho 14/10/2017 ifuatayo ni histor...
-
Mvutano huu umeendelea kuwa mkubwa zaidi pale rais wa Marekani bwana Donald Trump alipoamua kumtolea lugha chafu mwenzake wa N.Korea bwana ...
-
Kuelekea mechi ya Mbao FC dhidi ya mnyama mkali Simba SC historia ya timu hizi ni kama ifuatavyo Timu hizi ktk historia zao zimekutana mara...
No comments:
Post a Comment