Yanga iliundwa mwaka 1935 wakati Simba ikiundwa mwaka 1936 ikiwa Simba ni ya watoto wa kitajiri na Yanga ikiwa ni ya watoto wa kiafrika wa wenyeji. Timu hizi pinzani ndizo timu kongwe zaidi Tanzania na zenye historia kubwa pia.
Tangu ilipoanzishwa ligi ya taifa ya Tanzania 1965 ambayo sasahivi inajulikana kama ligi kuu Vodacom, timu hizi zimekutana mara 121 ktk michezo mbali mbali ikiwemo mechi za kirafiki, kombe la FAT, Headex cup, Tusker Cup,FA, Klabu bingwa Africa mashariki na kati, mtani jembe, ligi kuu na kadhalika.
Katika mapambano yote hayo Yanga imefanikiwa kuibamiza Simba mara 44 wakati Simba ikiichapa Yanga mara 43 huku zikienda sare mara 34.
Yanga ndio timu ya kwanza kuifunga Simba ktk mchezo wa kwanza kabisa bao 1-0 mwaka 1965 tarehe 07/06 na pia ikawa timu ya kwanza kuipiga simba magoli mengi zaidi katika historia yake mabao 5-0 mwaka 1968 tarehe 01/06.
Simba ilifanikiwa kujibu pigo hilo mwaka 1977 tarehe 19/07 kwa kuichapa Yanga bao 6-0 kipigo ambacho hakijawahi kujibiwa na watani zake Yanga kwa miaka 40 sasa. Pia simba ktk mchezo huo ilifanikiwa kupata mchezaji aliyefunga bao 3 peke yake maarufu kama Hattrick Abdallah Kibadeni jambo ambalo halijawahi kutokea tena miaka 40 sasa kwa mchezaji kufunga bao 3 peke yake kwenye mechi ya watani.
Simba kwa upande wake ni vinara wa kuwabugiza watani zao idadi kubwa ya magoli ktk mechi moja ambapo wamefanya hivi mara 4
19/07/1977 iliipiga yanga 6-0
02/07/1994 iliipiga yanga 4-1 mabao ya kwanza yote yakifungwa na centre half George Masatu kwa simba huku kwa yanga pia centre half Kimanda constantine akisawazisha lakini vijana wa simba walicharuka na kufunga mengine matatu kwa 4-1
18/04/2010 iliichapa yanga 4-3 sheikh amri abeid Arusha ukiacha mechi waliyowahi kutoa 4-4
06/05/2013 iliichapa yanga bao 5-0. Pia timu hizi zilishawahi kuweka mpira kwapani ambapo simba walifanya hivyo mara 2 na yanga mara 2
Yanga ina historia nzuri ya kuwa mabingwa mara nyingi zaidi ambapo wamebeba ubingwa mara 27 na simba mara 18 huku timu zingine zikichukua mara moja moja na zingine mara mbili tokea kuanzishwa ligi ya taifa mwaka 1965
Katika kuiwakilisha nchi Yanga imeiwakilisha nchi mara nyingi zaidi lakini simba ndio iliyoiwakilisha nchi kwa mafanikio zaidi ambapo mwaka 1974 ilitolewa nusu fainali ya klabu bingwa Afrika na Mehal el cubra ya Misri na kuifanya kuwa ndio timu pekee Tanzania iliyowahi kufika hatua ya nusu fainali klabu bingwa Africa. Simba pia mwaka 1993 ilifika hatua ya fainali kombe la shirikisho CAF na kutolewa na Stella Abdjan ya Ivory Coast ktk mchezo wa pili wa fainali kwa kufungwa bao 2-0 uwanja wa taifa Dar es salaam wakati ktk mchezo wa kwanza Abdjan Ivory coast zilitoka 0-0. Hivyo kuifanya kuwa ni timu pekee Tanzania kufika hatua hiyo ya fainali za CAF kombe la shirikisho
Simba pia ndio timu pekee Afrika mashariki na kati kuchukua kombe la klabu bingwa Afrika mashariki na kati kwa kulibeba mara 6 na kuifanya kuwa ni klabu pekee Tanzania na Afrika mashariki kulibeba kombe hilo mara nyingi zaidi.
Yanga kwa upande wake iliishia hatua ya makundi klabu bingwa Afrika mwaka 1998 na pia ikaishia hatua ya makundi kombe la shirikisho CAF 2016.
Kwa upande wa makocha waliopo sasahivi Joseph Omog wa Simba na George Lwandamina, rekodi zao zinaonyesha wamekutanana mara 4 wakiwa na timu hizi, mechi 2 za ligi kuu 1 ya kombe la mapinduzi na 1 ya ngao ya jamii. Lakini Omog ndiye ameibuka mbabe kwa kushinda mechi 3 huku Lwandamina akifanikiwa kupata sare 1.
Hata hivyo bado tunafanya tafiti za kina zaidi kujua ipi katika timu hizi yenye wapenzi na washabiki wengi zaidi ndani ya nchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Basi moja lijulikano kwa jina la LUJIGA limepata ajali eneo la Malendi mpakani mwa mkoa wa Singida na mkoa wa Tabora, Basi hilo lifanyalo...
-
Kuelekea mpambano wa ligi kuu soka Tanzania kati ya mnyama mkali simba sc na wana tamu tamu Mtibwa suger kesho 14/10/2017 ifuatayo ni histor...
-
Mvutano huu umeendelea kuwa mkubwa zaidi pale rais wa Marekani bwana Donald Trump alipoamua kumtolea lugha chafu mwenzake wa N.Korea bwana ...
-
Kuelekea mechi ya Mbao FC dhidi ya mnyama mkali Simba SC historia ya timu hizi ni kama ifuatavyo Timu hizi ktk historia zao zimekutana mara...

No comments:
Post a Comment