Monday, September 24, 2018

DERBY YA KARIAKOO, MPAMBANO MKALI KABISA WA WATANI WA JADI SIMBA Vs YANGA 30/09/2018


Kuelekea mpambano huu mkubwa barani Afrika Je wayajua mambo haya muhimu?       
 Huu ni mpambano wa kukata na shoka, ni miongoni mwa mipambano mikali zaidi barani Afrika ya watani wa jadi derby ukiacha mipambano kati ya Al ahly na Zamaleck za misri na ule wa Kaizer Chiefs na Orlando Pirates za Afrika kusini. Huu ni mpambano wa tatu kwa ukubwa barani Afrika. Ikumbukwe kuwa huu utakuwa ni mchezo wa 124 kama huna rekodi hiyo
    Katika michezo yote 123 iliyopita tangu mwaka 1965 rekodi zinaonyesha Simba imeitandika Yanga mara 44 na Yanga pia imeitandika simba mara 44 na wakenda sare mara 35 katika michezo yote zilivyokutana uso kwa uso. Pia ikumbukwe kuwa michezo hii yote 123 waliyowahi kukutana ni katika mashindano mbalimbali, ligi kuu Tanzania bara, ligi ya muungano wakati huo, kombe la FAT, Nyerere cup, Tusker cup, Hedex cup, klabu bingwa Afrika mashariki na kati kwa sasa Kagame cup, mtani jembe, mechi za kirafiki n.k.
    Katika mechi za ligi ligi kuu Tanzania bara peke yake utakuwa ni mchezo wa 101 ambapo katika michezo 100 iliyopita Yanga imeibuka wababe kwa simba kwa kuicharaza mara 35 huku simba ikiitandika Yanga mara 30 ilihali wakitoka sare mara 35. Kwa mantiki hiyo mechi hii huwa ni ya kusaka zaidi rekodi na kuweka heshima zaidi kuliko swala la pointi.
  Vile vile klabu hizi zote kila moja anatambia rekodi yake kwa mwenzake ambapo wengine wanasema tumebeba ubingwa mara nyingi zaidi na wenzao wanasema tunarekodi ya kushinda mabao mengi zaidi ktk mechi moja, lakini yote kwa yote tusubiri kuona nani ataibuka mbabe wa mwenzake. Kwetu sisi tuwaombee kila la kheri wote wacheze mchezo mzuri wa kiungwana bila kuwasahau waamuzi wazingatie vyema sheria za mchezo mwisho wa saa tupate mshindi aliyeshinda bila hila.

No comments:

Post a Comment

  Basi moja lijulikano kwa jina la LUJIGA  limepata ajali eneo la Malendi mpakani mwa mkoa wa Singida na mkoa wa Tabora, Basi hilo lifanyalo...