Sunday, May 6, 2018

Tarehe kama ya leo katika historia (May 06)

           Tarehe kama ya leo mwaka 2012 ilipigwa mechi kubwa ya watani wa jadi simba ikimkaribisha Yanga katika uwanja wa taifa Dar es salaam. Hii ilikuwa ni miongoni mwa mechi ya watani iliyokuwa na mabao mengi kabisa ukiacha ile ya 01/06/1968 na ile ya 19/07/1977 ambayo rekodi yake haijavunjwa hadi leo
         
          Mechi hii ya May 06,2012 simba iliikung'uta Yanga bao 5-0.
Bao la kwanza likiwekwa wavuni na Emmanuel Okwi dakika ya 2 tu ya mchezo huku Felix Sunzu Mzambia huyu akiweka kambani bao la pili kwa njia ya penalti dakika ya 56 ya mchezo.Dakika ya 62 ya mchezo Emmenuel Okwi tena akarudi kambani kwa mara ingine kuweka bao la tatu kufuatia uzembe wa mabeki wa yanga, huku Juma Kaseja akipachika bao la nne kwa njia ya penalti dakika ya 67 ya mchezo. Patrick Mutesa Mafisango akamalizia karamu ya magoli baada ya kuzifumania nyavu za Yanga katika dakika ya 72 ya mchezo na kuufanya mchezo uishie kwa 5-0 na kuifanya simba kubeba ubingwa msimu huo.

No comments:

Post a Comment

  Basi moja lijulikano kwa jina la LUJIGA  limepata ajali eneo la Malendi mpakani mwa mkoa wa Singida na mkoa wa Tabora, Basi hilo lifanyalo...