Friday, May 4, 2018
Ugeni uliotembelea Stendi kuu ya mabasi Singida (Misuna Terminal) toka Jumatano na Ijumaa East Africa Radio/EATV (channel5)
Ugeni huu wa East Africa radio na EATV ulitembelea kufanya mahojiano maalumu na uongozi wa stand kuu ya Misuna Terminal pamoja na wadau wa michezo wa misuna Terminal kutokana na kuvutiwa kwao na mambo mkubwa mawili
1. Kutokana na mpangilio,utaratibu na nidhamu ya hali ya juu ndani ya stand hii, walilazimika kuutafuta uongozi wa umoja wa mawakala angalau kupata darasa ni mbinu zipi au ni mambo gani yalifanyika kudhibiti mpangilio huu, utaratibu huu na nidhamu hii ya hali ya juu ambayo kwa mujibu wa maelezo ya wageni hawa hawajawahi kukutana na jambo kama hili stendi zote Tanzania. Ni jambo lisilopinginga kuwa ni kweli stendi nyingi Tanzania kama si zote hazina utaratibu mzuri wa kuhudumia jamii na kusababisha kero kubwa kwa wasafiri na watumiaji mbali mbali wa stendi hizo kiasi cha kusababisha kuitwa waizi, wahuni na walevi. Lakini kwa upande wa Stendi ya Singida Misuna Terminal, hili ni tofauti kabisa kiasi kwamba wageni hawa kuusifia sana kwa uongozi wa umoja wa mawakala kusimamia vyema utaratibu huu na nidhamu kwa wahudumu. Hivyo shukurani nyingi kwa wageni hawa East Africa Radio na EATV kwa kuliona hili na kuthamini jambo hili jema waliloliona na kuwajulisha umma wa Africa mashariki. Linaweza kuwa ni jambo la kuigwa na wengine kuondoa dhana mbaya kwa sekta hiyo ya huduma ya usafirishaji
2. Kutokana na kuvutiwa na idadi kubwa ya wadau wa michezo na washabiki wengi wa michezo na pia kujua maendeleo ya klabu ya Misuna Stand Football Club ambayo inamilikiwa na umoja wa mawakala,East Africa Radio/EATV walifanya mahojiano mbali mbali na viongizi wa chama cha soka cha wilaya, viongozi wa Misuna stand FC pamoja na wadau mbali mbali wa michezo waliokuwepo.Hata hivyo wadau wa michezo walifurahia ugeni huu kupitia kipindi chao cha KIPENGA EXTRA na kuomba watembelee mara kwa mara kwa maendeleo ya michezo nchini. Mapokezi ya wageni hawa yalienda vizuri na wadau wa michezo washukuru sana ujio huu wa ugeni kutoka East Africa Radio kwa kuwatembelea na kufanya ziara hizi mikoani kwa malengo ya kuibua changamoto mbali mbali na kuibua vipaji mbali mbali kama vipo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Basi moja lijulikano kwa jina la LUJIGA limepata ajali eneo la Malendi mpakani mwa mkoa wa Singida na mkoa wa Tabora, Basi hilo lifanyalo...
-
Kuelekea mpambano wa ligi kuu soka Tanzania kati ya mnyama mkali simba sc na wana tamu tamu Mtibwa suger kesho 14/10/2017 ifuatayo ni histor...
-
Mvutano huu umeendelea kuwa mkubwa zaidi pale rais wa Marekani bwana Donald Trump alipoamua kumtolea lugha chafu mwenzake wa N.Korea bwana ...
-
Kuelekea mechi ya Mbao FC dhidi ya mnyama mkali Simba SC historia ya timu hizi ni kama ifuatavyo Timu hizi ktk historia zao zimekutana mara...


No comments:
Post a Comment